Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa shirika la habari la SAFA, Mahmoud Abbas alituma ujumbe huo jana Jumamosi na kumsisitizia Rais Bashar al Assad kwamba taifa la Palestina limefurahi kuona wananchi wa Syria wamempa kura zao tena na kuelezea matumaini yake kuwa mataifa mawili ya Palestina na Syria yataendeleza juhudi zao za kidugu za kupigania maslahi na manufaa yao ya pamoja.
Ikumbukwe kuwa, serikali ya Syria imekuwa na mchango mkubwa katika kulilinda na kulihami taifa la Palestina na ni kwa sababu hiyo ndio maana Syria imefanyiwa njama kubwa na mabeberu wa dunia na vibaraka wao na kumiminwa mamia ya maelfu ya magaidi kutoka kila kona za dunia ili kwenda kufanya jinai dhidi ya wananchi na maafisa wa serikali ya Syria.
Kabla ya hapo pia Rais Michel Aun wa Lebanon alikuwa amemtumia salamu za pongezi Rais Bashar al Assad kwa kupata ushindi mutlaki katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni ndani na nje ya Syria ambapo baada ya kutangazwa kwake mshindi, watu wa miji yote ya Syria walijitokeza kwa maelfu kusherehekea ushindi, ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais huyo kwa kuiendesha vizuri nchi hiyo katika kipindi kizito na kigumu mno cha uvamizi wa magaidi na madola ya kibeberu.
Juzi Ijumaa, Spika wa Bunge la Syria alitangaza kuwa, Rais Bashar al Assad amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo kwa kupata zaidi ya asilimia 95 ya kura za wananchi.
342/